Benjamin Netanyahu na juhudi za kuyafufua mazungumzo ya amani | NRS-Import | DW | 09.11.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

NRS-Import

Benjamin Netanyahu na juhudi za kuyafufua mazungumzo ya amani

Israel yatangaza ujenzi wa makaazi mapya mashariki ya Jerusalem

default

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Israel inaendelea na mipango yake ya kutaka kujenga makaazi mapya 1300 ya walowezi wa kiyahudi  katika eneo la Jerusalem mashariki.

Tangazo la waziri wa mambo ya ndani wa Israel Efrat Orbach kuhusu mpango wa ujenzi wa makaazi mapya ya walowezi wa kiyahudi huko mashariki ya Jerusalem limetoa sura ya aibu mbele ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ambaye yuko Marekani katika juhudi za kutafuta njia ya kufufua mchakato wa amani na wapalestina.

NO FLASH Nahost Friedensgespräche in Washington

Marekani inakosoa ujenzi wa makaazi mapya katika ardhi ya wapalestina

Marekani imesema imevunjwa moyo na msimamo huo wa serikali ya Israel kwa kuwa ni hatua inayodhoofisha juhudi zote za kuyafufua mazungumzo ya moja kwa moja baina ya Waisraeli na Wapalestina.  Netanyahu pia atakuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton siku ya Alhamisi ambapo suala hilo bila shaka linatarajiwa kuibuka. Netanyahu pia alikutana hapo jana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye kwa mujibu wa ofisi ya habari ya Umoja wa Mataifa amezungumzia wasiwasi wake kuhusiana na tangazo la Israel.

Aidha Wapalestina wamelitaja tamko la Israeli kama ni uchokozi unaolenga kuvuruga juhudi za kusaka amani katika eneo hilo.Suala la ujenzi wa makaazi ya walowezi katika ardhi ya wapalestina inayokaliwa kwa nguvu na Waisrael limekuwa chachu ya mvutano kati ya pande hizo mbili kwa muda mrefu.

Mazungumzo ya moja kwa moja baina ya pande hizo  yalivunjika mwezi Septemba muda mfupi baada ya kuanzishwa, hatua iliyotokana na ukaidi wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wa kukubaliana na pendekezo la Palestina la kumtaka asimamishe ujenzi wa nyumba mpya za wayahudi Ukingo wa Magharibi. Msaidizi wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameondoa uwezekano wa kuridhia kuingia katika mazungumzo na Israel ikiwa nchi hiyo itaendelea kujenga katika ardhi yake na kuutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati na kuichukulia hatua Israel.

Grafik Symbolbild Franzöische Blauhelmsoldaten im Libanon UN-Soldaten UNIFIL Libanon UN-Mission Grafik UN-Fahne

Jeshi la Umoja wa Mataifa UNIFIL katika bandari ya mji wa Naqoura katika mpaka wa Israel na Lebanon

Ama kwa upande mwingine  Netanyahu amemwambia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwamba nchi yake ina mpango wa kuondoa wanajeshi wake kutoka eneo la mpakani na Lebanon na kukabidhi hatamu kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Lebanon UNIFIL limekuwa likiibinya Israel kuondoka katika kijiji cha Ghajar kuambatana na maagizo ya azimio nambari 1701  la baraza la usalama la Umoja huo ambalo lilisababisha kumalizika vita vya mwaka 2006 kati ya Israel na kundi la Hezbollah.

Mwandishi Saumu Mwasimba/AFPE

Mhariri Josephat Charo

 • Tarehe 09.11.2010
 • Mwandishi Saumu Ramadhani Yusuf
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Q2Fp
 • Tarehe 09.11.2010
 • Mwandishi Saumu Ramadhani Yusuf
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Q2Fp

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com