Benazir Bhutto hatotishwa na mashambulizi
20 Oktoba 2007Matangazo
Bhutto amesema,shambulizi hilo ni dhidi ya demokrasia, umoja na uadilifu wa Pakistan.
Mshambulizi aliejitolea maisha muhanga,alijiripua kati kati ya umati uliokuwa ukimkaribisha Bhutto kwa shangwe kubwa,aliporejea Pakistan baada ya kuishi uhamishoni kwa miaka minane iliyopita. Zaidi ya watu 130 waliuawa na kama 250 wengine wamejeruhiwa.Bhutto binafsi hakuumia.
Wanamgambo wenye itikadi kali za kiislamu wamelaumiwa na serikali kuhusika na shambulizi hilo ambalo ni baya kabisa kupata kufanywa nchini Pakistan.