1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE:Mustakabal wa Kosovo kujadiliwa

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaQ

Wajumbe wa Umoja wa Ulaya,Marekani na Urusi wanafanya mazungumzo na viongozi wa Serbia ili kuanzisha tena majadiliano kuhusu mustakabal wa jimbo lililojitenga la Kosovo.

Frank Wisener wa Marekani,Alexander Botsan-Kharchenko wa Urusi naye Wolfgang Ischinger wa Umoja wa Ulaya wanaendehsa mazungumzo hayo ya kulitafutia ufumbuzi suala la Kosovo.Wajumbe hao wanatarajiwa kukutana na viongozi wa Kosovo walio na asili ya Albania mjini Pristina hapo kesho.

Marekani inataka Kosovo kuwa na uhuru kamili wa kujitawala ili kumaliza shughuli za ujumbe wa kusimamia jimbo hilo.Hatua hiyo aidha itairuhusu Kosovo kupata mikopo ya kimataifa badala ya misaada ili kuimarisha uchumi wake.

Urusi iliyo na kura ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inapinga uhuru huo kwani inadai kuwa jimbo hilo ndio chimbuko lake.Jimbo la Kosovo lina wakazi wengi zaidi wa asili ya Albania.Kosovo imekuwa ikisimamiwa na Umoja wa mataifa tangu mwaka 99.Mjumbe wa Umoja wa mataifa wa zamani katika mazungumzo yaliyokwama Marti Ahtissari alipendekeza uhuru wa jimbo hilo.