1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELGRADE : Hakuna mshindi wa viti vingi bungeni

22 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYv

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge nchini Serbia yanaonyesha chama cha Serbia Radical kimejisombea kura nyingi sana.

Chama hicho cha msimamo mkali wa kitaifa kimejisombea viti 81 katika bunge lenye viti 250 lakini hakitokuwa katika nafasi ya kuunda serikali. Chama cha Demokratik kinachoungwa mkono na mataifa ya magharibi kimejipatia viti 65 na kushika nafasi ya pili.Nafasi ya tatu imeshikiliwa na chama cha Kihafidhina cha Demokratik cha Waziri Mkuu wa Serbia Vojislav Kostunica kwa kujipatia viti 48 wakati chama cha G17 Plus kimejipatia viti 19.

Kwa jumla vyama hivyo vitatu vina viti 132 ikiwa ni wingi wa viti bungeni lakini hakuna uhakika kwamba vyama hivyo viko tayari kushirikiana na kuunda serikali ya mseto.

Uchaguzi huo umefanyika ikiwa ni siku chache kabla ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuwasilisha mpango wake juu ya mustakbali wa jimbo la Serbia la Kosovo lenye waakazi wengi wa asili ya Kialbania ambalo limekuwa chini ya hemaya ya Umoja wa Mataifa tokea mwaka 1999.