BEIT HANUN : Mashambulizi ya Israel huko Gaza yalaaniwa | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIT HANUN : Mashambulizi ya Israel huko Gaza yalaaniwa

Wapalestina 18 wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa wakati makombora yaliposhambulia nyumba zao huko Gaza leo hii katika shambulio lililolaniwa na jumuiya ya kimataifa na uongozi wa Palestina.

Vifo hivyo na vya Wapalestina wengine watano waliouwawa katika shambulio la kabla ya alfajiri katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel na mwengine mmmoja katika kambi ya wakimbizi ya Gaza vimemfanya Rais wa msimamo wa wastani wa Palestina Mahmoud Abbas kuishutumu Israel kwa kuharibu nafasi za kuleta amani na kwa Hamas na Fatah kutowa wito wa kurudia mashambulizi ya kujitolea muhanga maisha.

Wakati viongozi wa Israel wakielezea masikitiko yao kwa maafa hayo na kuwa tayari kutowa msaada wa kibinaadamu kwa majeruhi jumuiya ya kimataifa imetowa wito wa kusitishwa kwa operesheni hiyo ya Gaza ambayo imeuwa zaidi ya Wapalestina 300 tokea kutekwa nyara kwa mwanajeshi wa Israel hapo mwezi wa Juni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com