1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIT HANOUN.Askofu wa zamani Desmond Tutu kuongoza tume ya uchunguzi

30 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoG

Mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani ya umoja wa mataifa Desmond Tutu atauongoza ujumbe wa umoja huo katika mji wa Beit Hanoun huko Ukanda wa Gaza utakaochunguza mauaji ya raia 19 mapema mwezi huu.

Mauaji hayo yalifanywa na majeshi ya Israel.

Askofu huyo wa zamani wa Cape Town nchini Afrika Kusini na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka 1984 anatarajiwa kuwasilisha ripoti juu ya mauaji hayo kwa tume ya haki za kibinadamu yenye makao yake katika mji wa Geneva, Uswisi katikati ya mwezi December.

Mapema mwezi huu kamati ya anchi 47 ilipitisha azimio la kulaani vitendo vya kukiukwa haki za binadamu na Israel katika ardhi iliyovamia.

Kamati hiyo ilipitisha kwamba uchunguzi ufanyike kuhusu mkasa wa Beit Hanoun.

Israel imesema imesikitishwa na mauaji hayo ya Novemba 8 lakini wakati huo huo ikawatwika lawama wapiganaji wa Palestina.