1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Wanamgambo 4 wauawa Nahr el-Bared

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSm

Vikosi vya serikali ya Lebanon vimewaua wanamgambo 4 wengine katika kambi ya wakimbizi ya Wapalestina kaskazini mwa nchi. Wanajeshi 2 pia walijeruhiwa katika mapambano hayo ya siku ya Jumatatu.Vikosi vya serikali,siku ya Jumapili, vilifanikiwa kumaliza uasi wa mwisho wa kundi la Fatah al-Islam katika kambi ya Nahr el-Bared.Hata hivyo,milio ya risasi na miripuko ilikuwa ikisikika karibu na kambi hiyo.

Katika mapigano ya mwisho,si chini ya wanamgambo 39 wa Fatah al-Islam waliuawa.Kwa mujibu wa duru za kijeshi,hadi wanamgambo 163 wameuawa,tangu kambi hiyo kuzingirwa na vikosi vya serikali kwa siku 105 zilizopita.