1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Wanajeshi wa jeshi la umoja wa mataifa wauwawa.

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoa

Wanajeshi sita wa jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa wameuwawa kwa bomu lililotegwa ndani ya gari kusini mwa Lebanon. Mlipuko huo , unaoaminika kuwa ni shambulio la kujitoa muhanga, umesababisha vifo vya wanajeshi wawili wa Hispania na watatu kutoka Colombia waliomo katika kikosi cha Hispania katika ujumbe wa umoja wa mataifa wa kulinda amani wa jeshi la mpito nchini Lebanon, UNIFIL.

Mmoja kati ya wanajeshi watatu wa Hispania waliojeruhiwa katika shambulizi hilo alifariki kutokana na majareha.

Muda wa jeshi hilo la mpito la kulinda amani UNIFIL uliongezwa baada ya vita vya mwaka jana vya siku 34 kati ya majeshi ya Israel na wanamgambo wa Hizboullah kusini mwa Lebanon.

Shambulio hilo limekuja baada ya watu kumi, ikiwa ni pamoja na wapiganaji sita wa kundi la Kiislamu, kuuwawa katika mapambano katika mji wa kusini wa bandari wa Tripoli siku ya Jumamosi.