1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Vikosi vyapambana upya na wanamgambo wa Fatah al-Islam

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBj6

Mwanajeshi mmoja wa Lebanon ameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka pamoja na wanamgambo wa Fatah al-Islam,waliojificha katika kambi ya wakimbizi ya Nahr al-Bared,kaskazini mwa nchi. Wakati wa mapambano ya hii leo,majeshi ya serikali yalishambulia vituo vya wanamgambo waliokuwa wakivurumisha makombora ya Katyusha kwenye vijiji vya jirani.Vikosi vya serikali, tangu tarehe 20 mwezi Mei,vinapambana na wanamgambo wa Fatah al-Islam.Juma hili,Waziri Mkuu wa Lebanon,Fuad Siniora alisema,anayataka majeshi yake yakomeshe uasi wa wanamgambo hao, katika kambi ya Nahr al-Bared.