1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Uchaguzi waahirishwa.

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK8

Uchaguzi wa rais nchini Lebanon umeahirishwa kwa mara ya tatu. Spika wa bunge Nabih Berri amesema katika taarifa kuwa uchaguzi huo umeahirishwa kutoka Jumatatu hadi tarehe 21 mwezi huu. Amesema kuwa hatua hiyo ina lengo la kutoa muda kwa wabunge kukubaliana juu ya mgombea atakayechukua nafasi ya Emile Lahoud, ambaye muda wake unamalizika Novemba 24. hapo kabla vikao vya bunge , mwezi wa Septemba na mwezi uliopita , vilishindwa kupata idadi inayohitajika kutokana na kususia kwa upande wa upinzani.