1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Uchaguzi waahirishwa.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E0

Bunge la Lebanon litachelewesha uchaguzi wa rais wiki ijayo ili kuruhusu muda zaidi kwa makundi hasimu pamoja na yale yanayoipinga Syria kukubaliana juu ya mgombea wamtakae.

Hii ni mara ya pili uchaguzi huo kuahirishwa , uchaguzi ambao utampata rais atakayechukua nafasi ya rais wa sasa Emile Lahoud. Kiongozi huyo anayeungwa mkono na Syria anatarajiwa kuacha madaraka hayo hapo Novemba 25.

Mapema siku ya Jumamosi mawaziri watatu wa umoja wa Ulaya walitembelea majeshi ya umoja huo nchini Lebanon yaliyowekwa kwa ajili ya ujumbe wa umoja wa mataifa wa kulinda amani kusini mwa nchi hiyo.

Bernard Kouchner wa Ufaransa , Massimo D’Alema wa Italia na Miguel Angel Moratinos wa Hispania walikutana na viongozi wa Lebanon mjini Beirut.

Mazungumzo yao yalilenga katika kumaliza mkwamo wa kisiasa ambao umeidhoofisha nchi hiyo kwa zaidi ya mwaka sasa.