1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Siniora asema Lebanon itaepuka mgogoro uliopo

10 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkW

Waziri Mkuu wa Lebabon Fouad Siniora ameapa kwamba serikali yake itaepukana na changamoto inayotokana na maelfu wa wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Kishia la Hezbollah kuandamana mjini Beirut kushinikiza kun’gatuka kwa serikali ya yake inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi.

Akizungumza ndani ya ofisi za serikali huku maelfu ya wapinzani wakiendelea kukusanyika jijini kwa siku ya kumi mfululizo amesema Lebanon ni nchi madhubuti na kwamba wataepukana na mgogoro huo.Siniora amesema hawataki Lebanon iwe jukwaa la vita vya wengine na kwamba wataulinda umoja wao na uhuru.

Waziri Mkuu huyo pia hakuupa uzito mgawiko unaopendelea nchini humo kwa kusema kwamba hakuna talaka baina ya Walebanon na kusisitiza wito wake wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya kambi mbili zinazofarakana ile inayoiunga mkono Syria na ile dhidi ya nchi hiyo

Upinzani unatowa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa kusema hawaitambuwi tena serikali hiyo baada ya kujiuzulu kwa mawaziri sita wanaoiunga mkono Syria mwezi uliopita.