1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Machafuko huenda yakazuka kaskazini mwa Lebanon

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz7

Afisa wa cheo cha juu wa kundi la kipalestina lenye siasa kali ameonya leo kwamba ikiwa jeshi la Lebanon litafanya kampeni ya kuwafurusha wanamgambo wa kiislamu walio katika kambi ya wakimbizi wa kipalesina, machafuko mabaya yatatokea.

Serikali ya Lebanon imeliamuru jeshi liwachakze wanamgambo wa kundi la Fatah al Islam walio ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nahr el Bared, ambako wapalestina elfu 31 wanaishi nje ya mji wa bandari wa Tripoli kaskazini mwa Lebanon.

Takriban wapiganaji 50 wameuwawa tangu mapigano yalipozuka Jumapili iliyopita.

Msemaji wa wizara ya ndani ya Marekani, Sean Mc Cormark, amesema, ´Kwa sasa tunatafakari juu ya ombi la kuongeza msaada kutoka kwa baraza la mawaziri la Lebanon na jeshi la Lebanon ambalo liko katika mapigano makali.´

Maelfu ya watu wamekuwa wakikimbia kutoka kambi ya wakimbizi iliyo kaskazini mwa Lebanon kufuatia siku tatu za mapigano makali kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa kiislamu.

Walioshuhudia wanasema wakaazi wengi wametumia muda mfupi yaliposita mapigano kukimbia, baada ya usitishwaji mapigano kutangazwa rasmi.