1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Wawili wauwa na tetemeko la ardhi

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBv4

Takriban watu wawili wameuwawa na watu wengine 70 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi lenye vipimo vya rishta 6.4 kukumba eneo la kusini magharibi mwa China.

Shirika la habari la Xinhua limearifu kuwa tetemeko hilo limeukumba mji wa milimani wa Pu’er katika mkoa wa Yunnan karibu na mpaka wa Laos na Burma.

Majumba kadhaa yameharibiwa na jitihada za kuwahamisha maelfu ya wakaazi wa mji huo zinaendelea.

Mawasiliano ya simu yameharibiwa kabisa kufuatia tetemeko hilo la ardhi.