1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Watu 94 wauwawa na mafuriko na maporomoko ya ardhi

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkg

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosabishwa na mvua kubwa yameuwa kiasi cha watu 94 na wengine 25 kutoweka katika mikoa saba nchini China.

Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa Xinua,takriban watu nusu millioni wameondolewa kwenye mikoa ya Jiangsu,Anhui,Henan,Hubei,Sichuan na Shaanxi na mji wa Chongqing.

Zaidi ya nyumba 49 elfu zimeharibiwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwenye maeneo yaliyoharibiwa vibaya ya Sichuan na Shaanxi.