BEIJING:mwandishi aachiwa baada ya miaka mitatu | Habari za Ulimwengu | DW | 15.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING:mwandishi aachiwa baada ya miaka mitatu

China imemwachia mwandishi wa gazeti la New York Times baada ya kuwa jela kwa takriban miaka mitatu.

Mwandishi huyo-Zhao Yan ambaye ni raia wa China alikamatwa mnamo mwaka 2004 na baadae alishtakiwa kwa kutoa siri za nchi.Jumuiya za kutetea haki za binadamu pamoja na nchi za magharibi zililaani kukamatwa mwandishi huyo.

Licha ya mashtaka juu ya kutoa siri za nchi kufutwa mwandishi huyo alipatikana na hatia ya udanganyifu wa fedha na alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com