1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:Korea kaskazini kufunga kinu chake kikuu cha nuklia

3 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKS

Korea kaskazini imekubali kutangaza mipango yake yote ya nuklia aidha kufunga kinu chake kikuu ifikapo mwisho wa mwaka huu chini ya usimamizi wa marekani.Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya makubaliano ya pande sita iliyotolewa hii leo.Makubaliano hayo ambayo ni awamu ya pili ya hatua za kumaliza mpango wa nuklia wa Korea kaskazini yamepokelewa vizuri na Rais George Bush wa Marekani aidha washiriki wengine katika mazungumzo hayo,Japan na Korea Kusini.

Chini ya awamu hiyo ya pili Korea Kaskazini itafunga kinu chake cha kuzalisha madini ya plutonium aidha viwanda viwili muhimu vya Yongbyon ifikapo Disemba 31.Viwanda vyengine vya Yongbyon vilishafungwa mwezi Julai katika awamu ya kwanza ya makubaliano ya mwezi Februari. Hata hivyo ripoti ya leo haujaelezea urutubishaji wa madini ya uranium ambao Marekani inashuku kuendelea.Korea kaskazini itapokea msaada wa nishati ambao kwa sasa imeshapokea tani laki moja za mafuta.