1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING:China yalalamikia hatua ya Washsington ya kumtunukia tuzo Dalai Lama

18 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ej

Utawala wa China umewasilisha rasmi kutoridhika kwake na hatua ya serikali ya mjini Washington ya kumtunukia mtawa Dalai Lama tuzo ya dhahabu ya bunge yenye hadhi kubwa nchini Marekani.

Rais George Bush na spika wa baraza la wawakilishi bibi Nancy Pelosi walimtunukia tuzo hiyo kiongozi huyo wa kidini wa Tibet katika dhifa maalum mjini Washington.

Rais Bush amemtaja kiongozi huyo wa kidini kuwa ni mfano wa amani na ustahamilivu na ameitaka serikali ya Beijing kumkaribisha na kufanya naye mazungumzo.