1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing.China na Ufaransa zataka vikwazo vya silaha dhidi ya Beijing viondoshwe.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz8

China na Ufaransa kwa mara nyengine tena, zimeutolea mwito Umoja wa Ulaya uondoshe vikwazo vya silaha dhidi ya beijing vilivyowekwa na Umoja huo.

Kufuatia mazungumzo yao yaliofanyika katika mji mkuu wa China, Beijing, Rais wa Ufaransa Jacques Chirac na kiongozi wa China Hu Jintao wamesema, maendeleo nchini China, yamefanya vikwazo vya kijeshi kutekelezeka vizuri.

Vikwazo hivyo viliwekwa mnamo mwaka 1989 kufuatia jeshi la china kuwauwa waandamanaji katika uwanja wa Tiananmen.

Viongozi hao wawili pia, wameelezea wajibu wao kuhusu suala la silaha za kinyuklia za Korea ya Kaskazini na kutaka zichukuliwe hatua za kidiplomasia ili kusuluhisha mzozo huo.