1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Tetemeko la ardhi lasababisha hasara China

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvG

Hadi watu 3 wameuawa na takriban 300 wengine wamejeruhiwa katika tetemeko kubwa la ardhi lililotokea kusini-magharibi ya China.Tetemeko hilo lililokuwa na nguvu ya 6.4 katika Kipimo cha Richter,lilitokea katika eneo la milimani kwenye mkoa wa Yunnan karibu na mipaka ya Laos na Burma. Ripoti zinasema,nyumba nyingi zimebomoka na mawasiliano ya simu yameathirika katika eneo hilo.Inasemekana kuwa kama watu 120,000 huenda wakahamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika vibaya sana.