1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Rais Köhler ziarani China

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzI

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler, yumo ziarani nchini China, kituo chake cha pili katika ziara ya wiki moja barani Asia. Rais Köhler amepangiwa kukutana na rais wa China, Hu Jintao na waziri mkuu Wen Jiabao.

Anatarajiwa kutumia mazungumzo yake na viongozi hao kuendeleza biashara kati ya Ujerumani na China, lakini wakati huo huo kueleza wasiwasi wake juu ya hali ya haki za binadamu nchini China.

Rais Horst Köhler aliwasili mjini Beijing akitokea nchini Vietnam alikofanya ziara ya siku mbili.