1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Mvua kubwa zasababisha mafuriko kusini mwa China

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBp7

Hadi watu 49 wamefariki katika mafuriko na mmomonyoko wa ardhi uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kusini mwa China.Katika mji wa Chongqing na wilaya za Hubei,Sichuan na Guizhou watu 23 wanakosekana.Kiasi ya watu milioni 10 wameathirika na zaidi ya wakazi 400,000 wamehamishwa sehemu zingine.Watu 128 pia walipoteza maisha yao juma lililopita katika mafuriko yaliyotokea sehemu zingine za eneo la kusini nchini China.