1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing: Makamu wa rais na wengine wawili waondolewa kamati kuu.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dt

Wanasiasa watatu wa ngazi ya juu nchini China wameondolewa katika kamati kuu ya chama tawala cha Kikoministi. Hatua hiyo imekuja mnamo siku ya mwisho ya mkutano mkuu wa chama unaofanyika kila baada ya miaka mitano. Shirika la habari la China Xinhua limeripoti kwamba wanasiasa hao ni makamu wa rais Zeng Qinghong, Luo Gann na Wu Gauanzheng. Aidha mkutano huo mkuu umeidhinisha pia mpango wa maendeleo ya kisayansi wa rais Hu Jintao. Mpango huo unalenga katika kuoanisha ukuaji uchumi na zingatio la hifadhi ya mazingira. Mkutano huo ukitarajiwa pia kumchagua tena Bw Hu kuwa kiongozi wa chama hicho kikoministi kwa miaka mitano mengine.