BEIJING :Indonesia na Uchina kuchimba mafuta Sudan | Habari za Ulimwengu | DW | 02.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING :Indonesia na Uchina kuchimba mafuta Sudan

Makampuni ya serikali ya Uchina na Indonesia wametia saini makubaliano ya kuchimba mafuta nchini Sudan kwa mujibu wa gazeti moja la Uchina.Ripoti hiyo inatolewa huku jamii ya kimataifa ilikalumu Uchina kwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwenye sekta ya mafuta nchini Sudan.Hatua hiyo inaaminika kuiwezesha Sudan kukataa shinikizo za mataifa ya kigeni katika suala la umwagikaji wa damu kwenye eneo la Darfur.

Mkataba huo wa miaka ishirini wa kuchimba mafuta unahusisha kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Uchina na PT Pertamina ya Indonesia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com