1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: China yaitaka Iran ishirikiane na shirika la IAEA

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLr

China imeitaka Iran iongeze ushirikiano wake na shirika la kimataifa la kuzuia utapakazaji wa silaha za kinyuklia, IAEA, huku dola kuu duniani zikiendelea kuibinya serikali ya Tehran isitishe mpango wake wa nyuklia.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa China, Li Zhaoxing, amesisitiza msimamo wa nchi yake kwamba juhudi za kidiplomasia zinatakiwa kupewa kipaumbele badala ya kusisitiza vikwazo ili kuishawishi Iran iachane na mpango wake wa nyuklia. Kiongozi huyo amesema hatua zitakazochukuliwa na Umoja wa Mataifa zinatakiwa kuendeleza ustawi wa kikanda.

Wakati huo huo, waziri Li Zhaoxing amesema China inataka amani na bajeti ya jeshi lake iko wazi. Aidha Zhaoxing amesema China inalinda haki zake na maslahi yake na inaheshimu haki na masilahi ya mataifa mengine. Matamshi yake yanafuatia hatua ya Marekani kuikosoa China kwa kuimarisha vikosi vyake.

Wakati haya yakiriafiwa rais wa China, Wen Jiabao, ameahidi kuchukua hatua za kuhifadhi nishati kuyalinda mazingira na kupunguza tofauti za kimaisha nchini mwake.

Rais Wen Jiabao aliyasema hayo jana wakati alipoufungua mkutano wa mwaka wa bunge la China.