1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beijing. China kuongeza matumzi ya kijeshi.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMC

China inapanga kuongeza matumizi yake ya kijeshi kwa zaidi ya asilimia 18 mwaka huu. Msemaji wa baraza la taifa la watu wa China alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing . Jiang Enzhu amesema kuwa licha ya kuwa ongezeko hilo ni kubwa , matumizi ya kijeshi yanabaki kuwa kama yalivyokuwa kwa mujibu wa asilimia ya matumizi jumla ya serikali. Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya China kueleza upinzani wake kwa mipango ya Marekani kuiuzia Taiwan makombora 450 ya angani na ardhini. China inaiona Taiwan kama jimbo lake lililojitenga.

Wakati huo huo China inampango wa kupunguza hali ya mtengano kati ya utawala wa nchi hiyo na wananchi wa kawaida. Akizungumzia hali hiyo waziri mkuu Wen Jiabao amewashutumu viongozi wa serikali kwa kujitenga na wananchi na pia kutumia vibaya madaraka yao. Kwa upande wa ulinzi wa mazingira waziri mkuu Jiabao amesema kuwa serikali yake itajitahidi kuwabana wale wanaokiuka kanuni za ulinzi wa mazingira.

Katika mwaka huu kutokana na mahitaji ya nishati tunataka kupunguza uharibifu wa mazingira na kubadilisha mtazamo ulioletwa na ukuaji wa kiuchumi. Makampuni ambayo bado hayajafuata utaratibu, uzalishaji wake utazuiliwa na hata kufungwa kabisa.