1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bei ya umeme yapanda Zanzibar

22 Mei 2012

Wakati gharama za maisha zinazidi kupanda kila siku Zanzibar serikali ya visiwa hivyo imepandisha bei ya umeme kwa asilimia 85 ambapo wananchi watalazimika kulipia huduma ya umeme kuanzia tarehe mosi mezi ujao.

https://p.dw.com/p/14zjT
Kollege Mohammed Abdulrahm hat sie gerade aus Sansibar geschickt und überlässt der DW das Copyright.
Makamo wa Rais Seif Sharif Hamad na Rais Dr.Ali Mohamed SheinPicha: DW

Zanzibar yenye idadi ya watu wanaokisiwa zaidi ya million moja, ina watumiaji wa umeme zaidi ya laki moja na elfu tano. Kasi ya matumizi ya Umeme Zanzibar imekuwa ukiongezeka kila mara kutokana na matumizi ya nishati hiyo kuongezeka pamoja na kampeni za kutaka wananchi watumie zaidi umeme na kupunguza ukataji miti ili kuepuka uharibifu wa mazingira. Mwandishi wetu Salma Said ametuandalia taarifa ifuatayo.(Kusiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini).

Mwandishi: Salma Said
Mhariri: Saumu Mwasimba