1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bei ya maziwa kupanda

1 Agosti 2007

Kupanda kwa bei ya maziwa na siagi Ujerumani,kumeongoza kudai wakulima nao kupandisha hata bei ya nyama.

https://p.dw.com/p/CHSG

Gazeti la Stuttgarter zeitung Laandika:

“je,wakulima hawakuwa hadi karibuni wakilaumiwa kuwa ni waroho wa kuzalisha mazao kupita kiasi mradi tu wanalipwa fidia kufanya hivyo ?

Soko likashughulikia haraka tena zaidi kuliko ilivyotazamiwa kurekebisha mezani ya bidhaa za kilimo masokoni na mahitaji halisi ya bidhaa hizi ili mezani ya nguvu ibadilike (kuwa sio bidhaa zinapindukia mahitaji).

Kwavile, huu sio mtindo wa muda mfupi,sera za kilimo za Umoja wa Ulaya mjini Brussels, nazo zapaswa kubadilishwa ili mageuzi yalioanza

Yaweze kuharakishwa.”

Ama Handelsblatt kutoka Düsseldorf,laandika:

“Mtu hawezi kuamini:Kwani wakulima wa Ujerumani hali zao ni nzuri sana.Bei za mazao ya kilimo zimekuwa zikipanda katika takriban kila upande.Mustakbala wa wakulima ni mzuri kabisa una nawiri.

Hali zao zinatiwa dosari na silaha ya kuwaumiza ya Umoja wa Ulaya.Kuwaamulia viwango maalumu vya kutoa maziwa –silaha inayotumiwa na Brussels tangu 1984.”

Ama kwa jicho la BERLINER ZEITUNG, uamuzi wa wakulima kupandisha bei ya maziwa na siagi una athari zake ulimwenguni:Laandika:

”kwa wakulima na sio tu Ulaya bali hata Marekani kupanda kwa bei ya maziwa na mazao yanayotokana nayo,ni matumaini mazuri.Hata wakulima masikini barani asia,Amerika Kusini na pengine hata Afrika ,kunaibuka fursa mpya za kunufaika.

Kwani, wakulima alfu 10 wa mahindi nchini Mexico wamepoteza mnamo miaka michache iliopita mapato yao kwavile hawakuweza kushindana na unga wa mahindi unaofidiwa kutoka Marekani kwa mlo wao wa Tortilla.”

Laandika Berliner Zeitung:

Ama gazeti la DIE WELT halipendezewi kabisa na kupandisha bei za maziwa na siagi.Lasema:

“Mjadala motomoto juu ya kupandisha bei ya maziwa na siagi unachukua sura ya kutastanisha:kwani, baada ya hasira juu ya kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, sasa nchi nzima inalalamika juu ya kupanda kwa bei ya maziwa.Wanasiasa wanadai malipo ya wale wanaopokea ruzuku ya mfumo wa Hartz-IV yaongezwe nayo na hautapita muda ,tutasikia vilio kudai kuwekwa tangi la maziwa ya bure ukumbini mwa idara ya leba kwa wasiomudu kununua maziwa.”