1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern yatinga 16, Gladbach yazuiwa

Bruce Amani
2 Novemba 2016

Robert Lewandoswki alifunga mabao mawili na kuwa shujaa wa Bayern wakati walitoka nyuma na kushindsa 2-1 dhidi ya PSV Endhoven na kufuzu katika hatua ya mtoano kukiwa na mechi mbili za kuchezwa.

https://p.dw.com/p/2S35U
Championsleague PSV Eindhoven gegen Bayern München
Picha: GettyImages/AFP/J. Thys

PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich
(Arias 14', Lewandowski 34' pen., 74')

Bayern ilijinyanyua kutokana na msururu wa bahati mbaya nyumbani kwa Eindhoven jana usiku na kutinga hatua ya 16 za mwisho ya Champions League kutoka Kundi D

Kwanza Robert Lewandowski alipiga mwamba wa goli baada ya Eindhoven kuongoza mpambano huo kutokana na dosari za refarii. Santiago Arias alifunga kwa kichwa baada ya kipa wa Bayern Manuel Neuer kukoa mpira wa kichwa kutoka kwa Davy Pröpper, lakini mfungaji huyo alionekana wazi kuotea. Bayern kisha wakajitajidi na kupata penalti iliyofungwa na Lewandowski. Mpira wa Joshua Kimmich ulionekana kuugonga mkono wa Andres Guardado na refarii akapeana penalti. Lewandowski alimaliza kazi kwa kufunga la pili katika kipindi cha pili.

Ijapokuwa vijana hao wa kocha Carlo Ancelotti ni wa pili katika kundi lao na pointi tisa nyuma ya Atletico Madrid ambayo ina pointi 12, wanafuzu pamoja na Wahispania hao huku Rostov na PSV zikiwa na pointi moja tu kila mmoja. Mapambano ya kumaliza kileleni mwa kundi yatakuwa katika michuano ya mwisho ya hatua ya makundi, wakati Bayern watakutana na Warusi Rostov Novemba 23.

Borussia Mönchengladbach 1-1 Celtic
(Stindl 32', Dembele 76' pen.)

Gladbach waliangukia pua kwa kukabwa na Celtic
Gladbach waliangukia pua kwa kukabwa na CelticPicha: Getty Images/Bongarts/S. Hofmann

Gladbach ilionekana kuwa katika udhibiti kuanzia mwanzo uwanjani Borussia Park lakini wakawaruhusu Celtic kuingia mchezoni na kuliacha Kundi C likiwa wazi. Celtic ambao walilazwa 2-0 na Wajerumani hao mwezi uliopita, hawakuonyesha mashambulizi yoyote katika dakika za mwanzo lakini wakasababisha hofu uwanjani baada ya Scott Sinclair kupiga shuti iliyogonga mwamba katikati ya kipindi cha kwanza. Hata hivyo Lars Stindl aliwafungia Gladbach bao la kwanza lakini dakika 15 kabla ya mchezo kukamilika, Moussa Dembele aliangushwa kwenye eneo la hatari na refarii akawapa penalty ambayo Dembele mwenyewe aliisukuma wavuni.

Ushindi wa Manchester City wa 3-1 wa nyumbani dhidi ya Barcelona sio habari nzuri kwa matumaini ya Gladbach kumaliza katika nafasi ya pili lakini wangali na nafasi maana imesalia mechi mbili. Barca wana pointi tisa, City saba, Gladbach nne na Celtic mbili. Gladbach watakuwa nyumbani dhidi ya City mnamo Novemba 23.

Matokeo ya mengine ya Jumanne katika Champions League:

Ludgorets 2-3 Arsenal (Arsenal imefuzu)

Basel 1-2 Paris St Germain (PSG imefuzu)

Besiktas 1-1 Napoli

Benfica 1-0 Dynamo Kiev

Manchester City 3-1 Barcelona

Atletico Madrid 2-1 Rostov (Atletico imefuzu)

Mwandishi: Bruce Amani/DW
Mhariri: Iddi Sessanga