Bayern Munich kileleni mwa Bundesliga | Michezo | DW | 24.09.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bayern Munich kileleni mwa Bundesliga

Wakati Bayern Munich imeparamia kileleni mwa Bundesliga, chelsea imeteleza mbele ya Manchester United katika premier League.Al Ahly ya Misri iko njiani kuvaa taji kwa mwaka 3 mfululizo katika kombe la klabu bingwa Afrika.

Mabingwa Stuttgart wazabwa 4:1 na Bremen

Mabingwa Stuttgart wazabwa 4:1 na Bremen

Wanariadha wa Kenya watia for a katika mashindano ya mwisho ya msimu huu wa riadha mjini Stuttgart Ujerumani;Chelsea yakomewa mabao 2:0 na mahasimu wao Manchester katika mpambano wao wa kwanza bila kocha Jose Mourinho,Bayern Munich yaizaba Karlsruhe 4-1 na kuparamia kileleni mwa Bundesliga.

Katika nusu-finali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika mabingwa Al Ahly ya Misri watoka suluhu 0:0 na Al-Ittihad ya Libya mjini Tripoli wakati Al Hilal ya Sudan yaizaba Etoile du sahel ya Tunisia 2:1 huko Oumduraman.

Mastadi 4 walioajiriwa msimu huu mpya na bayern Munich-mtaliana Luca Toni,mjerumani Miroslav klose,mturuki Hamit Alintop na mbrazil Ze Roberto, wote walipiga hodi katika lango la Karlsruhe,klabu ya zamani ya kipa wao Oliver Kahn na kukaribishwa ndani.

Kwa ushindi wa mabao 4-1 Bayern Munich imeanza msimu kwa vishindo ikitoa salamu kwa mabingwa Stuttgart kuwa huu si msimu wao kubakia na taji.Mabingwa Stuttgart,walichezrshwa kindumbwendumbwe na Werder Bremen na kukomewa pia mabao 4-1.

Hivi, ndivyo kocha wa mabingwa Stuttgart Armin Veh alivyosema baada ya pigo hilo:

“Kuwa leo tumefungwa ni tatizo dogo tu.tutabidi kuzungumza juu mambo muhimu yamchezo ulivyokwenda.Inatupasa nyuma kuwa imara na tutambe zaidi katika mpambano ya mtu na mtu na tukirekebisha hayo tutajikomboa katika hali ya sasa,kwavile tuna mastadi wa hadhi ya juu.”

Chelsea ilikiona jana kile kilichomtoa kanga manyoya ilipothubutu kuteremka uwanjani kucheza na mahasimu wao Manchester United bila kocha Jose Mourinho aliewaachamkono ghafula mapema wiki hii.

Chelsea ilizabwa mabao 2:0.Kocha wa muda Avram Grant,aliekuwa kocha wa taifa wa Israel, amesema punde si punde atathibitisha ni kocha aliefaa kujaza pengo la Jose Mourinho licha ya pigo la jana mbele ya Manchester.

Mashabiki wa Chelsea nchini Kenya wana maoni mengine kama mwanamichezo wetu Eric Ponda alivyogundua mitaani kwa mashabiki:

Nchini Tanzania,msimu mpya wa ligi umeanza na Chama cha mpira cha Zanzibar-ZFA- huenda kikashindwa kuandaa dimba la wasichana la kanda ya CECAFA.

Katika kinyan’ganyiro cha nusu-finali ya kombe la klabu bingwa barani Afrika,mabingwa Al Ahly ya Misri wametoka suluhu 0:0 na wenyeji Al Ittihad ya Libya mjini Tripoli,Al Hilal ya Sudan lakini iliizaba Etoile du Sahel ya Tunisia katika nusu-finali ya pili mabao 2:1.Washindi katika duru 2 za nusu-finali wakata tiketi za finali huku Al Ahly ikijiwinda kutwasa taji kwa mwaka 3 mfululizo.

Ama kwenye kinyan’ganyiro cha kombe la shirikisho la dimba la Afrika,Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imepigwa kumbo nqa kutolewa nje jana na TP Mazembe ya J.K.ya Kongo kwa mabao 3:1.

riadha:

Wanariadha wa Kenya walitamba jana katika finali ya msimu huu wa riadha-wiki 2 baada ya kumalizika ubingwa wa dunia huko Osaka: Stuttgart,kusini mwa Ujerumani, kitita cha dala milioni 3 kiligawiwa kwa washindi wa kwanza,wapili na watatu hapo jana:Katika mita 1500 Daniel Kipchircir Komen,alimkimbia Mehdi Baala wa Ufaransa kutwaa ushindi.Suleiman Kipses akabidi kuridhika na nafasi ya 3 na kitita cha dala 10.000.

Mshindi amenyakua dala 30.000 na wapili 20.000.Katika changamoto ya mita 3000 wakenya Edwin Soi na john Ebuja walichukua nafasi ya kwanza nay a pili wakimuachia Muhammed Farah aliekimbia kwa Uingereza nafasi ya tatu.

Ama katika mita 3000 kuruka viunzi,Wakenya waliondoka na kitita kizima pale Paul Kipsiele Koech ,Richard Matelong na Brimin Kipruto walipofuatana wa kwanza,wapili na watatu.Hata katika mita 5000 mambo yalikua zaidi ya hivyo huko Stuttgart:Edwin Soi,Macho Kogo na Moses Masai walitamba wakwanza,wapili na watatu.

Upande wa wanawake, bingwa wa dunia wa mita 800 Janeth Jepkosgei alitoroka na ushindi akifuatwa na Mayte Martinez wa Spain huku Marilyn Okoro wa Uingereza akifuata nafasi ya 3.

Katika changamoto ya mita 3000 wanawake, Meseret Defar wa Ethiopia alimtimua nje Vivian Cheruiyot na kuchukua ushindi.Vivian alibidi kuridhika na nafasi ya pili huku Prisca Jepleting akija 3 hapo.Katika mita 3000 kuruka viunzi,Eunice Jepkorir alifuata nyayo za wenzake wakiume na kuondoka na ushindi.

 • Tarehe 24.09.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHaz
 • Tarehe 24.09.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHaz