Baraza la waasi wa Libya lakutana na wajumbe wa kimataifa | Matukio ya Kisiasa | DW | 13.04.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Baraza la waasi wa Libya lakutana na wajumbe wa kimataifa

Baraza la Kitaifa la waasi wa Libya lawania kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa

default

Waziri wa mambo ya je wa Ujerumani Guido Westerwelle atahudhuria mkutano na wawakilishi wa Baraza la waasi wa Libya mjini Doha

Wajumbe wa Baraza la Kitaifa la waasi wa Libya leo wanakutana na wawakilishi wa kimataifa mjini Doha kuzungumzia juu ya kutambuliwa kwa Baraza hilo. Msemaji wa Baraza hilo ameeleza kuwa waasi wanatumai kutambuliwa ,hatua kwa hatua, kuwa wawakilishi halali wa Libya.Mpaka sasa Baraza la kitaifa linalowawakilisha waasi wa Libya linatambuliwa na Ufaransa,Italia na Qatari tu.

Jopo la kimataifa linalowasiliana na waasi wa Libya lililoundwa mjini London wiki mbili zilizopita, kwa mara ya kwanza litatafakari njia za kuleta amani nchini Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle pia atahudhuria mkutano huo wa mjini Doha. Wengine watakaohudhuria ni wawakilishi kutoka Umoja wa Ulaya,Umoja wa Mataifa,Marekani na kutoka Umoja wa nchi za Kiarabu.

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umeimarisha vikwazo dhidi ya utawala wa Kanali Gaddafi.Nchi za Umoja wa Ulaya zitazizuia akaunti za benki za makampuni 26 ya Libya na zitayapiga marufuku makampuni ya nchi za Umoja huo kufanya biashara na makampuni ya Libya.


 • Tarehe 13.04.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/10sCF
 • Tarehe 13.04.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/10sCF

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com