1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BARAZA LA USALAMA NA IRAN

24 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFr

UMOJA WA MATAIFA NEW YORK:

Baraza la Usalama la UM linatarajiwa masaa machache kutoka sasa kupitisha azimio litakaloiwekea vikwazo vipya Iran kuhusu ubishi wake unaohusiana na mradi wake wa kinuklia.Hii itafuatia azimio lililopitishwa na baraza la Usalama desemba mwaka jana lililoitaka Iran isimamishe kurutubisha madini yake ya uranium.

Hivi sasa taarifa zasema kwamba, rais Mahmoud Ahmadinejad amevunja safari yake aliopanga kwenda New York .Alitaka kulihutubia Baraza la Usalama kabla kura kupigwa hii leo.Mjumbe wa Iran katika UM amesema sababu ya kuvunja safari hiyo ni Marekani kuchelewesha kumpa viza ya kuingia Marekani tangu yeye hata na ujumbe wake.