1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la mawaziri bado halijatangazwa Kenya

Hamidou, Oumilkher6 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dcsw

Nairobi:

Kambi ya rais Mwai KIbaki wa Kenya na ile ya upande wa upinzani unaoongozwa na Raila Odinga hazijakubaliana bado juu ya muundo wa serikali ya umoja wa taifa .Serikali hiyo inayotazamiwa kua na mawaziri 40 ilikua itangazwe hii leo.Habari kutoka Nairobi zinasema hata hivyo huenda baraza hilo la mawaziri likatangazwa baadae leo mchana.Msemaji wa serikali amesema rais Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga watakutana hii leo kukamilisha masahauariano yao.Hitilafu za maoni zinakutikana katika suala la namna ya kugawana nyadhifa serikalini.Kambi ya rais Kibaki inawatwika jukumu la kucheleweshwa kutangazwa baraza la mawaziri,wafuasi wa ODM.Msemaji wa ODM amezisuta hoja hizo akisema chama chao kimeridhia mengi hadi sasa.Kufuatia maridhiano yaliyofikiwa kutokana na upatanishi wa mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika, katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan,raila Odinga anabidi akabidhiwe wadhifa wa waziri mkuu wa serikali mpya.