1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANGKOK: Miripuko ya mabomu yasababisha maafa nchini Thailand

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeD

Watu watatu wameuawa na wengine takriban thelathini wakajeruhiwa wakiwemo raia sita wa kigeni baada ya wimbi la mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Thailand, Bangkok.

Mabomu sita yaliripuka jana katika maeneo kadha ya mji huo na kusababisha serikali kufutilia mbali mipango ya kusherehekea mwaka mpya.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na miripuko hiyo lakini polisi wanaamini huenda wahusika ni wanamgambo wanaotaka kujitenga kusini mwa nchi hiyo.