BANGALORE.India yawasaka 12 wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulio ya Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BANGALORE.India yawasaka 12 wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulio ya Uingereza

Gazeti la kila jumapili la India limetoa taarifa kwamba polisi katika mji wa kusini mwa nchi wa Bangalore wamenzisha msako dhidi ya watu 12 wanaoaminika walihusika na mashambulio yaliyoshindwa nchini Uingereza.

Polisi wanasema wamepata CD kutoka nyumba za washukiwa wawili wa mashambulio hayo zinazoonesha juu ya mizozo inayowahusu waislamu katika jimbo la Chechniya na Iraq.

Watu wanane wengi wakiwa ni madaktari wanazuiliwa nchini Uingereza na Ausralia kuhusiana na majaribio ya kushambulia uwanja wa ndege wa Glasgow Scotland na London. Washukiwa hao wanatokea nchi za mashariki ya Kati na India.Bilal Abdullah ni mshukiwa wakwanza kushtakiwa jumamosi iliyopita kati ya washukiwa wanane.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com