1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki-moon kubadhiwa ripoti kuhusu Syria

14 Septemba 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema Ijumaa(13.09.2013) anaamini kutakuwa na ripoti inayoeleza wazi kutoka kwa wakaguzi wa silaha wa Umoja huokuwa silaha za kemikali zilitumika nchini Syria hapo Agosti 21.

https://p.dw.com/p/19hR3
SEOUL, SOUTH KOREA - AUGUST 23: UN Secretary-General Ban Ki-Moon speaks during the breakfast meeting hosted by diplomatic corps at Lotte Hotel Seoul on August 23, 2013 in Seoul, South Korea. (Photo by Chung Sung-Jun/Getty Images)
Katibu mkuu Ban Ki-moonPicha: Getty Images/Chung Sung-Jun

Katibu mkuu hata hivyo , hakusema nani anahusika.

Serikali ya Syria na waasi wanatupiana lawama kuhusiana na shambulio hilo lililofanyika katika kitongoji cha jiji la Damascus cha Ghouta. Utawala wa rais Obama , ambao unasema watu 1,429 wameuwawa, umeeleza kuwa una ushahidi ambao unaonesha wazi kwamba serikali ya Syria inahusika na shambulio hilo. Lakini Urusi, mshirika muhimu wa Syria, imesema haijashawishika na ushahidi wa Marekani.

epa03841638 A citizen journalism handout image provided by the Local Committee of Arbeen is said to show UN inspectors collecting samples during their investigations at Zamalka, east of Damscus, Syria, 29 August 2013. UN chemical weapons inspectors are to leave Syria 31 August morning, Secretary General Ban Ki-moon said. They would continue their investigations and would draw up a report as soon as they have left Syria, Ban said. On 29 August, they spent their third day in the field. EPA/LOCAL COMMITEE OF ARBEEN / HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FROM AN ALTERNATIVE SOURCE AND CANNOT PROVIDE CONFIRMATION OF CONTENT, AUTHENTICITY, PLACE, DATE AND SOURCE. HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES
Wataalamu wa silaha za kemikali wa Umoja wa Mataifa wakiwa SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Wakaguzi

Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wamepewa mamlaka ya kueleza iwapo silaha za kemikali zilitumika, na ni aina gani ya silaha hizo zilizotumika, lakini hawatakiwi kueleza nani anahusika. Hata hivyo wanadiplomasia wawili wa Umoja wa Mataifa wamesema ripoti hiyo inaweza kuelekeza kwa wale wanaohusika, akieleza kwamba wakaguzi wamekusanya sampuli nyingi kutoka katika eneo la shambulio na pia walifanya mahojiano na watu walioshuhudia.

Ban amezungumza muda mfupi kabla ya mkaguzi mkuu wa silaha za kemikali , Ake Sellstrom, kulieleza shirika la habari la Associated Press kuwa atawasilisha ripoti yake kwa katibu mkuu mjini New York mwishoni mwa juma hili. Wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa wamesema Ban anatarajiwa kulifahamisha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na ripoti hiyo siku ya Jumatatu asubuhi. Mwanadiplomasia huyo hakutaka kutajwa jina lake kwasababu muda huo bado haujathibitishwa.

US Secretary of State John Kerry gestures as his Russian counterpart Sergei Lavrov tries to fix his translation equipment during a joint press conference following their meeting in Moscow on May 7, 2013. The United States and Russia today agreed to push both warring sides in the Syria conflict to find a negotiated solution and to hold an international conference in search of peace. AFP PHOTO / POOL / MLADEN ANTONOV (Photo credit should read MLADEN ANTONOV/AFP/Getty Images)
Sergei Lawrow (kulia) na John Kerry(kushoto)Picha: AFP/Getty Images

Wakati huo huo Afisa mwandamizi wa ujasusi nchini Marekani, amesema Marekani imefikia idadi yake ya watu waliouwawa katika shambulio hilo katika eneo la Ghouta kwa kutathmini video zilizorekodiwa saa chache baada ya shambulio hilo na kuhesabu idadi ya watu ambao wanaonekana kuwa wamefariki katika shambulio hilo la gesi ya sumu, ikiwa ni pamoja na miili ambayo imefunikwa na ambayo haina damu , ikiwa ni ishara huenda hawakufariki kutokana na shambulio la kombora ama silaha nyingine zilizotumika katika shambulio hilo.

Matumaini yaongezeka

Vile vile wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka Marekani na Urusi wameongeza matumaini ya kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza vita vya muda mrefu na ambavyo vimemwaga damu nchini Syria, hata kama bado wanahangaika kushughulika na sehemu mbaya ya majadiliano hayo ya matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya raia.

Njia kuelekea kupata azimio la Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuziweka silaha hizo katika mikono ya jumuiya ya kimataifa inaonekana kuwa haina vikwazo tena, wakati Marekani inaonesha kuwa inaweza kukubaliana na hatua ya udhibiti ambayo haitishii kuchukua hatua ya kijeshi.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov , wakiongoza mazungumzo mjini Geneva kuzuwia mzozo huo , wote wameweka wazi uwezekano wowote wa kuanza tena kwa majadiliano mapana ya amani yanategemea kwanza kusuluhisha mkwamo kuhusiana na silaha za kemikali.

Mawaziri hao wawili wanatarajiwa kukutana tena leo Jumamosi,(14.09.2013).

epa03861918 President Barack Obama addresses the nation in a live televised speech from the East Room of the White House in Washington, DC, USA, 10 September 2013. President Obama blended the threat of military action with the hope of a diplomatic solution as he works to strip Syria of its chemical weapons. EPA/EVAN VUCCI / POOL
Rais Barack ObamaPicha: picture-alliance/dpa

Marekani ili kuimarisha hatua ya rais Bashar al-Assad ya kukabidhi silaha kama alivyoahidi , ikiwa ni pamoja na kuadhibiwa iwapo hatatekeleza.

Wakizungumzia kuhusu suala gumu linaloleta mkwamo, maafisa wa utawala wa Marekani wamesema kuwa rais Barack Obama yuko wazi katika kupatikana azimio ambalo halijumuishi matumizi ya kijeshi kama adhabu, ikiwa Urusi itakuwa na hakika kabisa bila ya kuipigia kura ya veto hatua yoyote ikiwa ni pamoja na adhabu kama hiyo.

Hata kama hatua ya kuiadhibu kijeshi Syria haitajumuishwa katika azimio la Umoja wa Mataifa , maafisa wamesema Obama ataendelea kuwa na mamlaka ya kuamuru shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya Syria.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Amina Aboubakar