1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban Ki Moon amtaka Gadaffi asitishe mashambulio

Thelma Mwadzaya7 Machi 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon,amemtaka kiongozi wa Libya,Kanali Muammar Gaddafi,asitishe vitendo vyote vya kuwashambulia raia wa kawaida.

https://p.dw.com/p/10UQG
Ban Ki-moon,Katibu Mkuu wa Umoja wa MataifaPicha: dapd

Kwa mujibu wa afisi yake ya mawasiliano,uongozi wa Libya huenda ukalazimika kuwajibika endapo utazikiuka sheria za kimataifa.Ili kuiweka sawa Libya,Ban Ki Moon amemteua waziri wa mambo ya nje wa Jordan wa zamani,Abdelilah Al-Khatib kuwa mjumbe maalum atakayeushawishi uongozi wa Libya kukaa katika meza ya mazungumzo ya dharura.

Azma ya mazungumzo hayo ni kulitafutia suluhu tatizo la wakimbizi wanaoyakimbia machafuko nchini humo. 

Flash-Galerie Rebellen in Libyen
Wapiganaji wanaompinga Kanali Gaddafi:Miji ya Misrata,Zawiya na Ras Lanuf inadhibitiwa na waasiPicha: dapd

Pindi waziri wa mambo ya nje wa Libya alipoiridhia mipango hiyo,Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa una mpango wa kuipelekea kundi maalum la wataalam watakaoitathmini hali halisi na mahitaji yake.Wakati huohuo,kuna hofu kuwa Libya huenda ikaingia katika kipindi cha vita vya wenyewe kwa wenyewe.Mapigano makali yameripotiwa kutokea pale vikosi vinavyomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi vilipojaribu kuiteka nyara miji ya Misrata,Az-Zawiya na Ras Lanuf inayodhibitiwa na waasi kwa sasa.