1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAMAKO : Afrika ina fursa ya kipekee kukuza uchumi

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCu2

Naibu Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF amesema hapo jana uchumi unoafaa duniani,msamaha wa madeni na maendeleo katika mageuzi ya kimuundo yanaipa Afrika fursa ya aina yake kuharakisha ukuaji wake wa kiuchumi.

Akizungumza katika ziara yake ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika tokea ashike wadhifa huo hapo mwezi wa Septemba naibu mkurugenzi mtendaji wa IMF John Lipsky amesema bara hilo linapaswa kunyakua fursa hiyo ya kufanya mageuzi zaidi ya kiuchumi.

Lipsky amesema huu ni wasaa maalum kwa Afrika akirudia kauli aliyoitowa hapo Alhamisi.

Amesema mchanganyiko wa mazingira mazuri ya nje, fursa zinazokuja kutokana na msamaha wa madeni na mafanikio ya mageuzi yanafunguwa njia kuelekea kipindi kipya au hata ukuaji mkubwa wa kiuchumi kwa watu wa nchi za Afrika.