1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAIDOA:Sehemu ya Majeshi ya Uganda yawasili Somalia

Kundi dogo la majeshi ya kulinda amani kutoka nchini Uganda yamewasili nchini Somalia.Maafisa hao waliwasili mjini Baidoa mapema hii leo ambao ni makao makuu ya serikali kwa muda baada ya kuwafurusha majeshi ya wapiganaji wa kiislamu mwezi Disemba mwaka jana.

Kulingana na afisa mmoja wa forodhani Ali Mohammed Adan aliyezungumza na shirika la habari la Reuters maafisa 35 kutoka Uganda wamefika nchini humo.

Serikali ya Uganda kwa upande wake inakanusha taarifa hizo.Uganda imekuwa na usiri mwingi kuhusu suala hilo la kupeleka majeshi nchini Somalia.Mpaka sasa bado haijasema tarehe hasa ya kutimiza ahadi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com