Baidoa: Mapigano yaendelea Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Baidoa: Mapigano yaendelea Somalia

Wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia yakiungwa mkono na wanajeshi wa Ethiopia wamepambana leo na wapiganaji wa muungano wa mahakama za Kiislamu ,saa chache baada ya kukamilika muda uliotolewa na muungano huo kuitaka Ethiopia iondowe majeshi yake katika ardhi ya Somalia au iwe tayari kwa mashambulio. Afisa wa wizara ya ulinzi mjini Baidoa alihakikisha kuzuka mapigano hayo katika mkoa wa Idale, kilomita 60 kusini mwa mji wa Baidoa yalipo makao makuu ya serikali ya mpito inayoongozwa na Rais Abdilahi Yussuf Ahmed.

Wakati huo huo halmashauri kuu ya umoja wa Ulaya , imetuma mjumbe wa ngazi ya juu mjini Baidoa kwa mazungumzo ya kujaribu kuepusha kupamba moto kwa mapigano. Habari zinasema Mjumbe huyo, ambaye ni kamishna wa maendeleo na misaada Louis Michel, alikua akikutana na Rais Abdilahi Yussuf Ahmed na Waziri mkuu Ali Mohamed Gedi na wakati yalipotokea mapigano katika vijiji viwili kandoni mwa Baidoa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com