1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Zaidi ya watu 30 wauawa nchini Iraq

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLY

Serikali ya Iraq imesema kuwa zaidi ya watu 30 wameuawa wakiwemo wanamgambo 18 katika mashambulizi yalitokea nchimi humo.

Katika Jimbo la Nineveh kaskazini mwa Iraq ambako kunakaliwa na wakristo wengi, bomu lililotegwa kwenye gari limeuwa watu wanne na kujeruhi wengine 16, ambapo katika mji wa Mosul imam wa Kisunni ameuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana.

Kwa upande mwengine jeshi la Marekani limesema kuwa limewaua wanamgambo 18 katika shambulizi lililofanyika kilomita 110 kaskazini mashariki mwa Baghdad.