BAGHDAD:Wanamgambo 40 wauwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 30.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Wanamgambo 40 wauwawa

Wanajeshi wa Iraqi wamewauwa wanamgambo 40 katika opresheni iliyofanyika kwenye mikoa mitatu kaskazini mwa nchi hiyo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Wizara ya ulinzi ya Iraq imesema opresheni hizo zimefanywa katika mikoa ya Diyala,Sallahudin na Kirkuk.Watu wengine wanane walikamatwa katika maeneo hayo.

Wakati huo huo wanajeshi wa Marekani pamoja na waIraq wamemkamata kiongozi wa juu wa mtandao wa kigaidi wa Alqaeda nchini Iraq Abdel Rahman al Anbary katika mji wa Sammara.

Anbary alikamatwa baada ya mapambano makali kati ya kundi lake na wanajeshi wa Marekani na Iraq ambapo wanamgambo 10 waliuwawa na wengine wanane wakajeruhiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com