1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Waandishi wa habari wauwawa Irak

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Fa

Mwandishi wa gazeti la Washington Post la Marekani wa nchini Irak na waandishi wengine wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi.

Salih Saif Aldin aliyekuwa na umri wa miaka 32 aliuwawa alipokuwa kazini katika kitongoji cha Sadaquiya mjini Baghdad.

Aldin atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika kupasha habari kutoka nchini Irak.

Katika kisa kingine kundi la watu waliokuwa na bunduki waliwafyatulia risasi waandishi wa habari wa gazeti la Salahaddin waliokuwa ndani ya magari mawili katika jimbo la Kirkuk.

Mwandishi mmoja ameuwawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kamati ya kuwalinda waandishi wa habari imesema kuwa takriban waandishi habari 118 wameuwawa nchini Irak.