1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Viongozi wa kikabila waapa kulipiza kisasi

14 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPq

Viongozi wa kikabila katika jimbo la Anbar magharibi mwa Irak wamelilaumu kundi la kigaidi la Al Qaeda kwa mauaji ya kiiongozi wao Abdul Sattar Abu Reesha.

Viongozi hao wamesema kwamba watalipiza kisasi.

Reesha aliuwawa katika shambulio la bomu la kutegwa kando ya barabara karibu na nyumbani kwake.

Alikuwa akiliongoza kundi la Anbar Awakenging Congerence lililokuwa mshirika wa Marekani katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Wiki iliyopiota rais Bush wa Marekani alikutana na Reesha na viongozi wengine wa kikabila wakati alipozuru nchini Irak.