1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Uwagikaji wa damu waendelea Iraq

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNf

Watu 10 waliuwawa hapo jana na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililotokeoa kwenye eneo la Bayaa karibu na mji wa Baghdad.

Polisi wamefahamisha bomu hilo lilitegwa ndani ya gari na kuripuka karibu na soko la kuuza mboga.

Vikosi vya Iraq na Marekani vilianzisha opresheni ya usalama wiki mbili zilizopita lakini wapiganaji wamekuwa wakiendelea na mashambulio takribana kila siku nchini humo.

Hata hivyo idara ya Afya nchini Iraq inasema idadi ya raia wanaouwawa kwenye mashambulio ya mabomu nchini humo imepungua kati ya tarehe mosi na tarehe 27 mwezi Februari.