BAGHDAD:Umjwagikaji damu waendelea Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 04.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Umjwagikaji damu waendelea Iraq

Wanajeshi wa Marekani wamewauwa wapiganaji 25 katika mashambulio ya angani ya siku tatu yaliyofanywa karibu na mji wa Baquba kiasi kilomita 65 kutoka kaskazini ya mji wa Baghdad.

Jeshi la Marekani limesema opresheni hiyo iliendeshwa karibu na mji wa Mukhisa mkoani Diyala na kwamba wanamgambo watano walikamatwa. Kwa mujibu wa jeshi hilo jumla ya watu 14 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji walikamatwa wakati wa uvamizi uliofanywa kwenye miji ya Baghdad na Mosul.

Wakati huo huo wanajeshi watatu wa Iraq wamejeruhiwa katika shambulio la kombora lilifanywa katika kambi yao iliyoko karibu na mji wa Hilla kusini mwa Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com