BAGHDAD:Shambulizi la kombora laua saba nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 18.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Shambulizi la kombora laua saba nchini Irak

Shambulizi la kombora pamoja na bomu la kutegwa kwenye gari limewaua watu saba na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa nje ya ofisi za Wizara ya Afya katikati ya Baghdad mapema leo

Milipuko zaidi imeripotiwa kutokea huko Mashariki na Kusini mashariki mwa Baghdad.

Wanamgambo wa Kisunni wameahidi kufanya kampeni za ghasia na mauaji kuadhimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika hatua nyingine wizara ya mambo ya ndani ya Irak imetangaza kuitimua nchini humo kampuni ya ulinzi ya kimarekani ya Blackwater.

Hii ni baada ya kutokea mauaji ya raia wanane wa Irak kutokana na risasi zilizofyatuliwa kutoka katika msafara wa walinzi wa kampuni hiyo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Condoleza Rice tayari amekwishaiomba radhi serikali ya Irak juu ya kitendo hicho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com