BAGHDAD.Rais wa Irak hospitalini baada ya kuugua | Habari za Ulimwengu | DW | 26.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD.Rais wa Irak hospitalini baada ya kuugua

Rais Jalal Talabani wa Irak amepelekwa mjini Amman, Jordan kwa matibabu baada ya kulemewa na uchofu mkubwa.

Ofisi ya rais mjini Baghdad imetoa taarifa kuwa hakuna sababu za kuwa na wasiwasi hata baada ya kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 74 kupelekwa hospitalini baada ya kiwango chake cha shinikizo la damu kushuka.

Mwanawe rais Talabani amesema kuwa baba yake yuko kwenye hali nzuri.

Habari zaidi kutoka Baghdad zinafahamisha juu ya kuuwawa takriban watu 50 katika shambulio la bomu.

Mshambuliaji anaeaminika kuwa ni mwanamke alijilipua nje ya chuo cha elimu na kusababisha vifo vya watu 40 na kuwajeruhi wengine 35.

Waziri mkuu Nuri Al Maliki anadai kuwa hali ya usalama imeimarika nchini Irak.

Nae mshauri wa maswala ya usalama nchini Irak Muwafak Al Rubaie ametoa kauli sawa na ya waziri mkuu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com