BAGHDAD:Nouri el Maliki azionya nchi zinazokosoa kunyongwa Saddam Hussein | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Nouri el Maliki azionya nchi zinazokosoa kunyongwa Saddam Hussein

Baghdad:

Serikali ya Irak imetangaza opereshini kubwa ya kijeshi dhidi ya waasi.Wanajeshi wa Irak wataanza kuwasaka waasi kijiji baada ya kijiji kuanzia leo.Vikosi vya serikali vitasaidiwa na wanajeshi wa Marekani.Wakati huo huo waziri mkuu wa Irak,Nouri El Maliki ametishia kuzingatia upya uhusiano wa nchi yake na zile nchi zilizokosoa kunyongwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein.Nouri El Maliki,ambae ni wa madhehebu ya shia amesema kunyongwa kiongozi huyo wa zamani wa Irak ni suala la ndani la Irak.Anahoji kesi na hukumu dhidi ya Saddam Hussein zimefanyika kwa haki na kunyongwa kwake ni kwa manufaa ya umoja wa Irak.Kanda ya video inayoonyesha jinsi Sadam Hussein alivyokua akitukanwa alipokua anatiwa kitanzi,na kumkatia shahada,imezusha hasira na kuzidisha mivutano nchini Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com