BAGHDAD:Ndege za jeshi la Marekani zauwa watu | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Ndege za jeshi la Marekani zauwa watu

Takriban watu 25 wameuwawa wakati ndege za kijeshi za Marekani ziliposhambulia kijiji cha Al Jaysani kilicho karibu na maeneo ya mji wa Al Khalis unaokaliwa na jamii ya Washia huko nchini Irak.

Shambulio hilo lilitokea mwendo wa saa nane usiku na kuasababisha uharibifu kubwa katika nyumba nne za raia.

Katika shambulio jingine la ndege za kijeshi za Marekani watu 17 wameuwawa wakiwemo wanawake na watoto karibu na mji wa Bakuba.

Taarifa kutoka wizara ya ulinzi mjini Baghdad imearifu kwamba watu 27 wamejeruhiwa katika shambulio hilo na watu wengine wanane hawajulikani walipo.

Awali jeshi la Marekani lilitoa taarifa kuwa limewauwa watu 25 ambao wanashukiwa kuwa ni wapiganaji wenye msimamo mkali wakati wa operesheni iliyolemlenga kamanda anaehusiana na Iran na ambae anaaminika kuhusika katika uingizaji silaha kupitia mpakani kati ya Irak na Iran.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com